ANZIA POPOTE, ILA JUA UENDAPO
Hii picha niliipiga mwaka mmoja baadae, Hapo nilikuwa Nimewaza kupata usaidizi wa ujenzi wa banda bora la kufugia kuku. Ilikuwa mwezi wa 4,mwaka 2017. Kiukweli ilinichukua muda sana kufanya ushawishi wa ujenzi wa banda kubwa lenye uwezo wa kutunza kuku 300-350. Kwa muda huu nilikuwa na idadi ya kuku wapate 180 kama jumla ya wote, wadogo kwa wakubwa.
Na huu ndio ulikuwa mwonekano wa mabanda yangu ya ufugaji wa kuku, ikiwa kama mradi wangu wa kwanza. Nguvu za mwili pamoja na nguvu ya akili viliweza kunipatia kidogo hicho na sikati tamaa wala kurudi nyuma.
Maisha ni jangamoto, kila jambo tufanyaro ni changamoto, kila siku, wiki, mwezi na mwaka vinakuja na changamoto zake. Kama binadamu hatuna budi kuvikabili maana Mungu alishatupa kila kitu kuanzia nguvu hadi akili.
Hivi leo kunavijana wanalia kwamba hawana pa kuanzia, hawana mitaji hivyo wanasubili siku wakipata mitaji ndo wajishughulishe, SIO SAHIHI, anza na ulichonacho mbele yako, mengine yatakuja taratibu, kama ilivyonichukua mwaka mzima kupata banda lenye hadhi nzuri. Anzia ulipo, usitazame Elimu yako, CERTIFICATE, DIPLOMA, DEGREE, MASTERS AU PHD, fanya ukipendacho bila kuangalia watu wanasemaje, mwisho watakuona /watashtuka tayari upo juu ya mlima wao bado wapo bondeni wakipiga story zako.
SEE YOU AT THE TOP,
MUTTA BUSINESS COMPANIES
Maoni
Chapisha Maoni