Machapisho

ANZIA POPOTE, ILA JUA UENDAPO

Picha
Hii picha niliipiga mwaka 2016 mwezi wa tatu nilipoanza rasmi kujiwekeza katika sekta ya kilimo na mifugo. Nilijikita katika ufugaji wa kuku wa kinyesi. Hilo ndo lilikuwa banda langu la kwanza likiwa na idadi ya kuku 20. Japo ilikuwa ngumu kushawishi ndugu na jamaa kuhusu wazo langu la kujikita katika sekta ya kilimo na mifugo, niliamua kuingia kama mimi bila ya kujali kama watu wanakubaliana na wazo langu au la! Nilijiamini kama mimi, japo sikuwa na kianzio chochote Cha kupanua mradi wangu.  Hii picha niliipiga mwaka mmoja baadae, Hapo nilikuwa Nimewaza kupata usaidizi wa ujenzi wa banda bora la kufugia kuku. Ilikuwa mwezi wa 4,mwaka 2017. Kiukweli ilinichukua muda sana kufanya ushawishi wa ujenzi wa banda kubwa lenye uwezo wa kutunza kuku 300-350. Kwa muda huu nilikuwa na idadi ya kuku wapate 180 kama jumla ya wote, wadogo kwa wakubwa.  Na huu ndio ulikuwa mwonekano wa mabanda yangu ya ufugaji wa kuku, ikiwa kama mradi wangu wa kwanza. Ng...